Misingi ya Imani ya Kanisa la ICC Mito ya Uzima

Kanisa la ICC tunaamini kwa dhati kuwa Biblia ndio Mwongozo wa Imani yetu na matendo katika maisha yetu ya Kikristo. Tamko hili ndilo msingi wa ushirika wetu (yaani, kwamba sote tunazungumza kitu kimoja, 1Kor.1:10; Mdo.2:42). Ukiri wa Imani yetu umejengwa katika misingi kumi na sita (16) ifuatayo:

1. Maandiko Yaliyovuviwa

Tunaamini kwamba Maandiko yote ya Agano la Kale na yale ya Agano Jipya yamevuviwa kihalisi na Mungu na ni Ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, ni mamlaka ya mwisho ya imani yetu na matendo katika maisha yetu ya Kikristo (2Tim.3:15-17; 1The.2:13; 2Pet.1:2)

2. Mungu Mmoja aliye Hai na wa Kweli

Tunaamini kwamba Mungu mmoja tu aliye hai na wa kweli amekwisha kujifunua mwenyewe kama “MIMI NIKO” wa milele, muumbaji wa mbingu na nchi na Mkombozi wa Ulimwengu na Wanadamu. Yeye pia amejifunua zaidi kama mwenye kufuata mwenendo na ushirikiano na uhusiano katika Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (Kumb. 6:4; Isa.43:10,11; Mat.28:19; Lk.3:22).

UUNGU UNAOPENDEZA

(a) Maneno Yamefafanuliwa

Maneno utatu na nafsi hai, kama yanavyohusiana na Mungu, ingawa hayapatikani katika Maandiko Moja kwa moja, ila dhana ya Utatu na nafsi hai imeenea ndani ya maandiko. Ni maneno yanayopatana na Maandiko, ambayo kwayo twaweza kuwafikishia wengine uelewa wetu wa haraka wa fundisho la Kristo kuhusu Mungu, linalo tofautishwa na “miungu wengi na mabwana wengi.” Kwa hiyo tunaweza kusema kwa hakika juu ya Bwana Mungu wetu, ambaye ni Bwana Mmoja, kama Utatu au kama Mungu mmoja katika nafsi hai tatu, na bado tuwe wa kimaandiko kabisa (mifano, Mathayo 28:19; 2 Wakorintho 13:14; Yohana 14:16,17).

(b) Tofauti na Uhusiano katika Uungu

Kristo alifundisha tofauti ya Nafsi katika uungu ambayo aliionyesha kwa maneno maalum ya uhusiano, kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, lakini kwamba tofauti hii na uhusiano, kuhusu hali yake ni isiyochunguzika na isiyoeleweka kikamilifu kwa akili za kibinadamu, kwa sababu haijafafanuliwa (Luka 1:35; 1 Wakorintho 1:24; Mathayo 11:25-27; 3: 24; 24; 19; 1:3,4).

(c) Umoja wa Mungu Mmoja wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu

Ipasavyo, kwa hiyo, kuna kile ndani ya Baba kinachomfanya awe Baba na si Mwana; kuna kile ndani ya Mwana kinachomfanya awe Mwana na sio Baba; na kuna kile ndani ya Roho Mtakatifu ambacho kinamfanya yeye kuwa Roho Mtakatifu na sio Baba au Mwana. Kwa hivyo, Baba ndiye Mzaa; Mwana ndiye Mzaliwa; na Roho Mtakatifu ndiye atokaye kwa Baba na Mwana.

Kwa hiyo, kwa sababu nafsi hizi tatu katika uungu ziko katika hali ya umoja, kuna Bwana mmoja tu Mwenyezi na jina lake moja (Yohana 1:18; 15:26; 17:11,21; Zekaria 14:9)

(d) Utambulisho na Ushirikiano katika Uungu

Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu hawafanani kamwe katika kuwa nafsi hai; wala kuchanganyikiwa katika kuhusiana; wala kugawanyika katika heshima ya uungu; wala kupingana katika kushirikiana. Mwana yuko ndani ya Baba na Baba yuko ndani ya Mwana kuhusu uhusiano. Mwana yu pamoja na Baba na Baba yuko pamoja na Mwana, kuhusu ushirika. Baba hatoki kwa Mwana, bali Mwana atoka kwa Baba kuhusu mamlaka. Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na Mwana akiendelea, kuhusu asili, uhusiano, ushirikiano, na mamlaka. Kwa hivyo, hakuna nafsi hai katika uungu ambayo ama ipo au inafanya kazi kibinafai au bila ya wengine (Yohana 5:17-30,32,37; 8:17,18).

(e) Cheo, Bwana Yesu Kristo

Jina la Bwana Yesu Kristo, ni jina sahihi. Haitumiki kamwe katika Agano Jipya ama kwa Baba au kwa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo ni mali ya Mwana wa Mungu pekee (Warumi 1:1-3,7; 2 Yohana 3).

(f) Bwana Yesu Kristo, Mungu Pamoja Nasi

Bwana Yesu Kristo, kuhusu asili Yake ya uungu na ya milele, ndiye Mzaliwa wa pekee anayefaa na wa pekee wa Baba, lakini kuhusu asili Yake ya kibinadamu, Yeye ndiye Mwana wa Adamu anayefaa. Kwa hiyo, anakubaliwa kuwa Mungu na mwanadamu; ambaye kwa sababu Yeye ni Mungu na mwanadamu, ni “Imanueli,” Mungu pamoja nasi (Mathayo 1:23; 1 Yohana 4:2,10,14; Ufunuo 1:13,17).

(g) Cheo, Mwana wa Mungu

Kwa kuwa jina Imanueli linajumuisha wote wawili Mungu na mwanadamu, katika nafsi hai mmoja, Bwana wetu Yesu Kristo, inafuata kwamba cheo Mwana wa Mungu kinaeleza uungu Wake ufaao, na cheo Mwana wa Adamu, ubinadamu Wake halisi. Kwa hiyo, cheo Mwana wa Mungu ni cha mpangilio wa umilele, na cheo Mwana wa Adamu kwa mpangilio wa wakati (Mathayo 1:21-23; 2 Yohana 3; 1 Yohana 3:8; Waebrania 7:3; 1:1-13).

(h) Ukiukaji wa Mafundisho ya Kristo

Kwa hiyo, ni uvunjaji wa fundisho la Kristo kusema kwamba Yesu Kristo alipata cheo Mwana wa Mungu kutoka kwa ukweli wa Umwilisho, au kwa sababu ya uhusiano Wake na gharama ya ukombozi. Kwa hiyo, kukataa kwamba Baba ni Baba halisi na wa milele, na kwamba Mwana ni Mwana halisi na wa milele, ni kukana tofauti na uhusiano katika Uungu wa Mungu; kukana kwa Baba na Mwana; na kuhamishwa kwa ukweli kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili (2 Yohana 9; Yohana 1:1,2,14,18,29,49; 1 Yohana 2:22,23; 4:1-5; Waebrania 12:2).

(i) Kuinuliwa kwa Yesu Kristo kama Bwana

Mwana wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu, malaika na enzi na enzi zikiisha kutiishwa chini yake. Naye akiisha kufanywa kuwa Bwana na Kristo pia, alimtuma Roho Mtakatifu ili sisi, katika jina la Yesu, tupige magoti na kukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba hadi mwisho, wakati Mwana atakapojitiisha chini ya Baba ili Mungu awe yote katika yote ( Waebrania 1:3; 1 Petro 3:22; Matendo 2:32-36; 2 Wakorintho 2:15; 2 Wakorintho 15:1;

(j) Heshima sawa kwa Baba na kwa Mwana

Kwa hiyo, kwa kuwa Baba amemkabidhi Mwana hukumu yote, si jukumu la wazi la wote walio mbinguni na duniani kupiga goti tu, bali ni furaha isiyoelezeka kwa Roho Mtakatifu kumpa Mwana sifa zote za uungu, na kumpa heshima na utukufu wote uliomo katika majina na vyeo vyote vya uungu isipokuwa zile zinazoonyesha uhusiano, (rejea Aya ya b, c, na d) na hivyo basi humheshimu Mwana kama vile sisi tunavyo mheshimu Baba. (Yohana 5:22,23; 1 Petro 1:8; Ufunuo 5:6-14; Wafilipi 2:8,9; Ufunuo 7:9,10; 4:8-11).

3. Uungu wa Bwana Yesu

Tunaamini kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na ana sifa zote za Uungu (Yoh.1:1; 8:58; Isa.9:6;1Yoh.5:20). Maandiko yanatangaza:

  • Kuzaliwa kwake na bikira (Mt.1:23;Lk.1:31:35).
  • Maisha yake yasiyo na dhambi (Ebr.7:26;1Pet.2:22).
  • Miujiza yake (Mdo. 2:22, 10:38)
  • Kazi yake ya malipizi juu ya msalaba (1Kor.15:3, 2Kor.5:21).
  • Ufufuo wake kimwili kutoka katika wafu (Mt.28:6; Lk.24:39, 1Kor.15:4).
  • Kutukuzwa kwake kwenye mkono wa kuume wa Mungu (Mdo.1:9; 11; 2:33; Fil. 2:9-11; Ebr.1:3).
4. Anguko la Mwanadamu

Tunaamini kwamba mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu akiwa mzuri na mwema, maana Mungu alisema: “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu”. Hata hivyo mwanadamu kwa uasi wa hiari yake mwenyewe alianguka na kwa njia hiyo akajiletea mauti siyo ya kimwili tu, bali pia mauti ya kiroho ambayo ni kutengwa na Mungu (Mwa.1:26, 27; 2:17; 3:6; Rum. 5:12-19).

5. Wokovu wa Mwanadamu

Tunaamini kwamba tumaini la pekee la mwanadamu la ukombozi ni kwa njia ya damu ya Yesu Kristo, mwana wa Mungu iliyomwagika.

(a) Masharti ya Wokovu

Tunaamini kwamba wokovu hupatikana kwa njia ya toba mbele za Mungu na imani kwa Bwana Yesu Kristo. Kwa kuoshwa kwa kufanywa upya na kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu, kuhesabiwa haki kwa neema kwa njia ya imani, mwanadamu hufanyika mrithi wa Mungu kulingana na tumaini la uzima wa milele (Lk.24:47; Yoh.3:3; Rum. 10:13-15; Efe. 2:8; Tito 2:11; 3:5-17).

(b) Ushahidi wa Wokovu

Tunaamini kwamba ushahidi wa wokovu ulio wa ndani ni ushuhuda wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu (Rum. 8:16). Ushahidi wa nje kwa watu wote ni ya haki na utakatifu wa kweli (Efe. 4:24; Tito 2:12).

6. Maagizo ya Kanisa

(a) Ubatizo katika Maji Mengi

Ubatizo katika Maji Mengi: Tunaamini juu ya agizo la ubatizo wa kuzamisha linatolewa katika Maandiko. Wote wanaotubu na kumwamini Kristo kama Mwokozi na Bwana wanaweza kubatizwa. Kwa njia hiyo, wanautangazia ulimwengu kwamba wao wamekufa pamoja na Kristo na pia kwamba wao wamefufuliwa pamoja naye ili kuenenda katika upya wa uzima (Mt.28:19, Mk.16:6; Mdo.10:47, 48; Rum. 6:4).

(b) Ushirika Mtakatifu

Tunaamini juu ya meza ya Bwana ambayo ina mkate na matunda ya mzabibu ni mfano wa kuelezea ushirika wetu wa asili ya ki-Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo (2 Pet.1:4). Ni kumbukumbu ya mateso yake na kifo chake (1Kor.11:26) na ni sharti kwa waamini wote hata ajapo.

7. Ubatizo wa Roho Mtakatifu

Tunaamini kwamba waamini wote wanatakiwa na wanayo haki ya kutafuta ahadi ya baba, yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu, kulingana na agizo la Bwana wetu Yesu Kristo. Huu ulikuwa ni ujuzi wa kawaida kwa wote waliokuwemo katika kanisa la mwanzo la Kikristo. Pamoja na huo ubatizo huja uwezo kutoka kule juu kwa ajili ya maisha ya utumishi, na kutolewa kwa karama pamoja na matumizi yake katika huduma (Lk.24:49; Mdo.1:4; 8; 1Kor.12:1-31). Ujuzi huu ni tofauti kabisa ingawa unalingana na ujuzi wa kuzaliwa upya (Mdo.8:12-17; 10:44-46;11:14-16; 15:7-9). Pamoja na ujuzi huo wa ubatizo katika Roho Mtakatifu kunakuja ujuzi mwingine kama kujazwa mpaka kufurika kwa Roho Mtakatifu (Mdo.2:43,Ebr.12:28), kujitoa kwa hali ya juu kwa ajili ya Mungu na kujiweka wakfu kwa ajili ya kazi yake (Mdo.2:42), pamoja na upendo wenye vitendo zaidi kwa Kristo na kwa Neno lake na kwa wanaopotea (Mk.16:20).

8. Ushahidi wa Ubatizo katika Roho Mtakatifu

Tunaamini kwamba ubatizo wa waamini katika Roho Mtakatifu unashuhudiwa kwa ishara ya nje iliyo ya kimwili ya kunena kwa lugha nyingine kama Roho wa Mungu anavyowajalia hao kutamka (Mdo.2:4). Huku kusema kwa lugha ni sawa sawa na ile karama ya aina za lugha (1Kor.12:4-10,28) ingawa ni tofauti katika makusudi na matumizi.

9. Utakaso

Tunaamini kwamba utakaso ni tendo la kutengwa na kile kilicho kiovu na kujiweka wakfu kwa ajili ya Mungu (Rum. 12:1,2; 1Thes. 5:23; Ebr.13:12). Maandiko yanatufundisha juu ya maisha ya utakatifu ambao pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Mungu (Ebr. 12:12-14). Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu sisi tunao uwezo wa kutii amri ile: “Iweni watakatifu kama mimi name nilivyo Mtakatifu” (1Pet. 1:15,16).

Utakaso huwa halisi katika mwamini kwa kugundua na kufahamu utambulisho wake na Kristo katika kifo chake na kufufuka kwake, na kwa imani akijihesabia kila mara kwamba yumo katika muungano huo, na kwa kutoa kila kiungo kila mara kwa utawala wa Roho Mtakatifu (Rum. 6:1-11;13; 8:12;13; Gal.2:20; Filp. 2:12; 13; 1Pet. 1:15).

10. Kanisa

Tunaamini kwamba kanisa ni mwili wa Kristo, makao ya Mungu kwa njia ya Roho, lenye vyeo vya ki-Mungu kwa ajili ya utimizo wa kazi yake kuu. Kila mwamini aliyezaliwa kwa Roho ni sehemu muhimu ya kanisa ambalo ni kusanyiko la wazaliwa wa kwanza walioandikwa Mbinguni (Efe.1:22;23; 2:22; Ebr.12:23).

Kwa kuwa kusudi la Mungu kuhusu mwanadamu ni kutafuta na kuokoa kile kilichopotea, kuabudiwa na mwanadamu, kujenga kusanyiko la waumini kwa mfano wa Mwanawe, na kuonesha upendo na huruma yake kwa ulimwengu wote, sababu za kipaumbele za kuwepo kwa ICC kama sehemu ya Kanisa ni:

(a) Kuwa wakala wa Mungu kwa ajili ya kueneza injili ulimwenguni kote. (Matendo 1:8; Mathayo 28:19,20; Marko 16:15,16).

(b) Kuwa chombo cha ushirika ambamo mwanadamu anaweza kumwabudu Mungu (1 Wakorintho 12:13).

(c) Kuwa njia ya Mungu kupitishia kusudi lake la kujenga kusanyiko la watakatifu wanaokamilishwa katika mfano wa Mwanawe (Waefeso 4:11-16; 1 Wakorintho 12:28; 14:12).

(d) Kuwa watu wanaoonesha upendo na huruma ya Mungu kwa ulimwengu wote (Zaburi 112:9; Wagalatia 2:10; 6:10; Yakobo 1:27).

Kanisa la ICC liko ili kuendeleza waziwazi msisitizo uleule wa sababu za kuwepo kwa muundo wa Kanisa la kitume la Agano Jipya kwa kufundisha na kuwatia moyo waumini kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Uzoefu huu:

(a) Huwawezesha kuinjilisha katika nguvu za Roho ikiambatana na ishara za nguvu za Mungu zisizo za kawaida (Marko 16:15-20; Matendo 4:29-31; Waebrania 2:3,4).

(b) Huongeza kipimo muhimu kinachohitajika katika uhusiano wa ki -ibada na Mungu ( 1 Wakorintho 2:10-16; 1 Wakorintho 12-14 ).

(c) Huwawezesha wasmini kuitikia utendakazi kamili wa Roho Mtakatifu katika kuonesha tunda na karama na huduma kama ilivyokuwa nyakati za Agano Jipya kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo na kuwajali maskini na wahitaji wa ulimwengu (Wagalatia 5:22-26; Mathayo 25:37-40; Wagalatia 6:10; 1 Wakorintho 11 Wakorintho 14:12; 12:28; Wakolosai 1:29;

11. Huduma

Tunaamini kwamba huduma ya ki-Mungu pamoja na utumishi uliopangwa na maandiko umetolewa na Bwana wetu kwa makusudi matano

12. Uponyaji wa Kimungu

Tunaamini kwamba uponyaji wa kimungu ni sehemu muhimu ya Injili. Kufunguliwa kutoka magonjwa na vifungo mbalimbali ni haki ya kila anayeamini (Isa. 53:4; 5; Mt.: 8:16;17; Yak. 5:14-16).

13. Tumaini lenye Baraka

Tunaamini juu ya ufufuo wa wale ambao wamelala katika Kristo na kunyakuliwa kwao pamoja na wale walio hai waliosalia mpaka wakati wa kuja kwake Bwana ndilo tumaini lenye baraka na lililo kuu la Kanisa (1Thes.4:16, 17; Rum. 8:23; Tito 2:13; 1Kor.15:51, 52).

14. Utawala wa Kristo wa miaka Elfu

Tunaamini kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni pamoja na kunyakuliwa kwa Watakatifu ambalo ni tumaini lenye baraka, kukifuatiwa na kurudi kwa wazi kwa Kristo pamoja na Watakatifu wake kwa ajili ya kutawala hapa Ulimwenguni kwa muda wa miaka elfu moja (Zek. 14:5; Mt. 24:27;30; Ufu.1:7; 19;11- 14; 20:1-6). Utawala huu wa miaka elfu moja utaleta wokovu kwa Israeli kama taifa (Eze. 37:21,22; Zef.3: 19, Zab. 72:3-8; Mika 4:3,4).

15. Hukumu ya Mwisho

Tunaamini kwamba kutakuwepo na hukumu ya Mwisho ambayo humo wafu waovu watafufuliwa na kuhukumiwa sawa sawa na matendo yao. Yeyote, ambaye hatakutwa ameandikwa katika Kitabu cha Uzima, pamoja na Shetani na malaika zake, mnyama na nabii wa uongo, watatupwa katika adhabu ya milele katika ziwa liwakalo moto na kibiriti, ambayo ni mauti ya pili (Mt. 25:46; Mk.9:43-48; Ufu. 19:20; 20:11-15; 21:8).

16. Mbingu Mpya na Nchi Mpya

Kulingana na ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya ambamo haki yakaa ndani yake (2Pet.3:13; Ufu. 21 na 22).

Kulingana na ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya ambamo haki yakaa ndani yake (2Pet.3:13; Ufu. 21 na 22).

swSwahili
Scroll to Top