Kuhusu ICC Mito Ya Uzima
Historia ya Kanisa la ICC Mito ya Uzima
Mnamo Septemba 2014, Kanisa la ICC Mito ya Uzima lilizaliwa katika sebule ndogo ya kawaida ya nyumba ya Mchungaji Emanuel Meshlyek katika mtaa wa Area Five, barabara CC, plot 172, nyumba namba 8, Manispaa ya Morogoro, Tanzania. Kile kilichoanza kama idadi ndogo sana ya waamini waliojitolea kwa moyo thabiti, kikawa pahala pa mafundisho ya Biblia yasiyoghoshiwa, sala na maombi ya bidii, semina za kuleta mabadiliko chanya kwa wanaookolewa, na ushirika wa kutoka moyoni. Likiwa na mizizi katika Neno la Mungu na kuchochewa na Roho Mtakatifu, kanisa lilikua kwa kasi huku mioyo ikichochewa na Injili.
Ndani ya miezi michache, sebule ndogo ya kawaida ilijaa waabuduo. Kadiri Mungu alivyo waongeza kiidadi kwa wale wanaookolewa, chumba cha chakula na kibaraza cha nje navyo vilijaa waabuduo kutoka kwetu Tanzania, Ethiopia, DRC Congo, Uganda, Kenya, Rwanda, Malawi, Za,mbia, Lesotho, Botswana, Japan, Msumbiji, China, Marekanii, Nigeria, na waamini kutoka mataifa mbalimbali - wengi wao wakiwa wanafunzi wa kimataifa katika vyuo vikuu hapa Morogoro. Ushirika huu ulijumuisha Umoja wa mwili wa Kristo kutoka mataifa mbalimbali.
Ili kushughulikia kusanyiko lililokuwa likiongezeka, kanisa lilijenga hema lake ndogo la kwanza kwenye ua wa mbele wa nyumba ya Mchungaji Emanuel. Hata chini ya hema hiyo, Mungu aliendelea kubariki huduma, akililazimisha kanisa kupanua muundo mara kwa mara. Sauti ya ibada, shuhuda, na mafundisho ya upako yasiyobadilika yalisikika zaidi ya hema, yakivuta roho zaidi katika ufalme wa Mungu.
Leo, ICC Mito ya Uzima inasimama ukingoni mwa sura mpya na yenye kuvutia sana. Kwa neema ya Mungu kanisa limefanikiwa kupata kiwanja chenye ukubwa wa ekari 2 na kidogo, katika manispaa ya Morogoro huku asilimia 90 ya malipo hayo yakiwa yamekamilika. Juhudi zinaendelea ili kuongeza 10% iliyobaki ili kukamilisha umiliki. Ardhi hii itatumika kama msingi wa kudumu wa kuendeleza ufalme wa Mungu kupitia huduma kamili. Mipango ya siku zijazo katika ardhi hiyo ni pamoja na:
- Jengo la ibada kwa lishe ya kiroho.
- Shule ya upandaji makanisa kuandaa viongozi.
- Shule ya Chekechea yenye lugha ya Kiingereza ili kusomesha na kufunza watoto.
- Kituo cha afya cha kuhudumia mahitaji ya kiafya ya jamii.
- Kisima cha maji safi kutatua shida ya ukosefu wa maji kwa jamii.
- Kituo cha Redio na kituo cha TV ya Kikristo ili kutangaza matumaini katika mikoa yote.
Tukiongozwa na maneno ya Zaburi 127:1 “Bwana asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi hukesha bure,” - ICC Mito ya Uzima inamwamini Mungu kutimiza mambo haya makuu kwa utukufu wake. Kwa pamoja, kanisa linasonga mbele, likiamini kuwa kile kilichoanza katika sebule ndogo ya kawaida kitaongezeka na kuwa urithi wa mabadiliko chanya kwa Morogoro na kwingineko ulimwenguni. Utukufu una yeye Mungu pekee, sasa na hata milele, Amina
KInasaba Chetu / Utamaduni wa Kukua kwetu
- Kukua katika Kimo kupitia ibada - Yoh 4:19-24; Ebr 10:25; 1Kor 1:21;
- Kukua katika joto la udugu kupitia ushirika Matendo 2:42, 44; Jn. 13:34, 35; Rum. 15:26;
- Kukua katika Kina kupitia uanafunzi Mt. 28:19,20; Kol. 1:9-11;
- Kukua katika Uimara kupitia huduma Lk. 4:18,19; Yoh 13:3, 14; Mt. 25:37-40;
- Kukua katika Kujieneza/ Mapana kwa njia ya Uinjilisti Matendo 1:8; Mt. 28:19,20; Mk. 16:15;
Tunachoamini
Kanisa la (ICC) lina mafundisho makuu manne ya msingi;
(i) Wokovu,
(ii) Ubatizo katika Roho Mtakatifu,
(ii) Uponyaji wa Kimungu na
(iv) Ujio wa Pili wa Kristo.
